Wivu
Inasemekana wanaume wafupi wana wivu wa kupindukia na sio kama wanaume wengine warefu hawana wivu ila wao wivu wao unapitiliza kiasi cha kukera kwani wivu ukizidi sana ni kero katika mapenzi.
Sifa
Wanaume wengi wafupi wana sifa sana, kiasi cha kukera wanajisifia sana, na wanataka sana kuonekana, kama wapo eneo Fulani wakiingia sehemu mtajua kama kuna mtu kaingia sababu ya sifa zao na maneno yao japokuwa pia wana sifa moja ya kuwa wacheshi sana.
Gubu
Hapa sasa ukichanganya na wivu ni balaaa maana mwanaume mwenye gubu ni zaidi ya mwanamke muongeaji, Gubu ni ile hali ya kukosoa kila kitu,kila kitu kibaya, yeye haridhiki na chochote na hata utaonekana huwezi chochote akiwa karibu, hilo gubu au hata kama kila kitu kipo sawa atatafuta sababu ya kuongea tu.
Wanajidai Wanajua kila kitu. ( Much know)
Much knows, hapa bwana unakutana na mtu kila kitu anajua yeye, ni kero sababu akiwa mbele za watu atataka kila mtu ajue anajua nini kama inaongelewa siasa, mpira au mapenzi yeye fundi wa kila kitu, kitu ambacho kiukweli kinakera sana wakati mwingine.
Muonekano/ Mvuto
Wanawake wengi wanasema wanaume wafupi hawana mvuto sana, kama wanaume warefu, kwahiyo hiyo ni moja ya sababu ya wao kutotaka kutoka na wanaume wafupi, japokuwa sio wanaume wote wafupi hawana mvuto. Japokuwa inasemekana siku hizi hakuna anaeangalia urefu wako uzuri wako watu wanangalia sana mfuko wako tu, hayo ni maneno ya mitaani watu wanaongea. Mimi binafsi sijui kama ni hali halisi.
0 comments:
Post a Comment